Tuesday 28 August 2018

Millard Ayo amfuata Ommy Dimpoz Afrika Kusini



Kupitia kipindi cha Amplifaya kinachorushwa kupitia Clouds FM , @millardayo amezungumza na mwanamuziki @ommydimpoz na kueleza juu afya yake.
.
.

@ommydimpoz ameiambia Amplifaya kuwa kwa sasa anaendelea na matibabu huku hali yake inazidi kuimarika.
.
.
Mkali huyu ambaye anasumbuliwa na tatizo la koo toka Mwanzoni mwa mwezi wa sita.
.
.
“Vipimo vya nchini Kenya vilionyesha kwamba ugonjwa wangu ulisababishwa na kunywa kitu chenye sumu, na wakasema ukubwa wa tatizo nililokuwa nalo itabidi niende kutibiwa nje,
"Ugonjwa huu wa matatizo kwenye mfumo wangu wa chakula umenianza siku nyingi kidogo, nimekuwa nikihangaika kwenye hosptali tofauti nchini Tanzania na kwa wakati tofauti nilikuwa napewa majibu tofauti. Wengine waliniambia koo langu limepata uvimbe na kusababisha kutoweza kupitisha chakula vizuri, wengine waliniambia nina kansa ya koo. Lakini nakumbuka wakati kipindi cha harusi ya Alikiba, nilikutana na Gavana Joho wa Mombasa na akanisaidia kunikutanisha na madaktari wengine nchini Kenya," amesema @ommydimpoz kupitia kipindi cha Amplifaya

0 comments:

Post a Comment