Wednesday 29 August 2018

Aretha Franklin aagwa na maelfu mjini Detroit



Mapema leo marehemu Aretha Franklin amepewa heshima za mwisho na maelfu ya watu waliojitokeza kwenye makumbusho ya kihistoria ya watu weusi 'Charles G. Wright' mjini Detroit leo Jumanne - Swipe kushoto kuona baadhi ya picha.

Malkia huyo wa Soul duniani alifariki mapema mwezi huu baada ya mapambano ya muda mrefu na ugonjwa wa saratani. Mwili wake uliingia taratibu viwanjani hapo kwenye gari aina 1940 Cadillac LaSalle ambayo ilitumika pia kuubeba mwili wa marehemu baba yake mzazi Mchungaji C.L. Franklin miongo kadhaa iliyopita.

Aretha anatarajiwa kuzikwa Ijumaa hii na huduma ya uimbaji itatolewa na Stevie Wonder pamoja na Jennifer Hudson.

0 comments:

Post a Comment