Thursday 2 August 2018

Polisi Zimbabwe wasaidiwa na jeshi kutuliza ghasia

  • Polisi wametumia maji ya kuwasha na mabomu ya machozi ili kuwatawanya Waandamanaji huku ndege za kijeshi zikizunguka angani.
    Hayo yametokea baada ya maelfu ya waandamanaji kudai kuwa uchaguzi uliofanyika umekuwa sio wa haki
    -
    Maandamano hayo yamefanyika nje ya makao makuu ya Tume ya Uchaguzi nchini humo(ZEC) ambayo inashutumiwa na wafuasi wa upinzani kuwa inaegemea upande mmoja kwenye uchaguzi huo
    -
    Waandamanaji wengine wameonekana kuwataka Rais Emmerson Mnangagwa na Makamu wake Constantino Chiwenga(Mkuu wa Jeshi wa zamani), kuachia ngazi mara moja
    -
    Wafusi wa vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo wa kihistoria siku ya Jumatatu wamekuwa wakionyesha hali ya kuchoka katika usubiriaji wa matokeo ya Urais

0 comments:

Post a Comment