Friday 3 August 2018

Cardi B awachana 'Haters' wake



Cardi B yupo real sana hasa pale linapokuja suala la kuwachana wabaya wake - kupitia ngoma zake au hata kuwajibu kwa mdomo na captions.

Leo tena #CardiB ameonekana kuwaonjesha mashabiki zake ladha ya dude jipya kupitia ukurasa wake wa instagram.

Kwenye video hiyo ambayo Cardi amei-post kwenye page yake, ameonekana ku-rap Bars kuntu straight kwa Haters wake kwenye wimbo ambao huwenda ukadondoka hivi karibuni.

"Do you hate my attitude or is just my appearance? / Are you mad I get paid just to make an appearance? / Are you mad your baby daddy wanna make me a parent? / I look good in everything Fashion Nova on Clearance" - ilisikika mistari ya Cardi B kwenye video - Swipe kushoto kuiona.

Wiki iliyopita rapper huyo alitudokeza kuhusu ujio wa kazi zake kuanzia mwezi ujao pamoja na kuiachia video ya 'Ring' aliyofanya na Kehlani.

0 comments:

Post a Comment