Friday 10 August 2018

Rais Durteret atangaza kuwaangamiza maofisa wahalifu



Rais Rodrigo Duterte ametishia kuwaua maofisa wa Jeshi la Polisi ambao wako chini ya uchunguzi kwa uhalifu katika hotuba iliyokuwa ikilenga wahalifu ndani ya Jeshi hilo

Duterte, Rais mwenye maneno ya kejeli, Jumanne aliwashambulia maofisa wa Polisi 102 akisema 'hawana maana na ni mzigo kwa jamii'

Majina ya maofisa wengi wa Polisi yako chini ya uchunguzi kwa makosa makubwa ya uhalifu yakiwemo ya ubakaji, kuteka, kupotosha na kujihusisha katika biashara ya dawa za kulevya

Duterte aliwaonya maofisa hao kwamba ikiwa wataendelea na vitendo vyao vya uhalifu na kugundulika basi watauawa

0 comments:

Post a Comment