Saturday 1 September 2018

Kampuni ya kifedha ya NALA yanyakua tuzo Togo



Kampuni ya Mtanzania Benjamin Fernandes (@benji_fernandes) ya @nala.money imeshinda tuzo ya Kampuni Bora ya Fintech Africa chini ya mwamvuli wa Bank ya Ecobank nchini Togo.

Nala ndio inakuwa kampuni ya kwanza kutoka Tanzania kushinda tuzo hiyo ya Ecobank Fintech challenge.

"Kwa Mara ya Kwanza katika historia kampuni ya kutoka Tanzania inashinda Tuzo hii. Tume zawadiwa kwa kuwa kampuni Bora ya #Fintech Africa 2018," ameandika Benjamin.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Benjamin ameeleza furaha yake na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi ili kuipokea tuzo hiyo inayoleta heshima nchini hasa katika maswala ya ubunifu.

"Ninayo furaha isiyo kifani kuwaletea Tuzo hii Nyumbani kwani ni zao la Tanzania. Kumbuka Mmoja akifika wote tume fika Mmoja akishangilia wote tumeshangilia. Mungu apewe sifa zote. Daima. πŸ™πŸΌπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ–πŸΎπŸ“±," amendika @benji_fernandes
.
.
Nala ni kampuni ya kwanza nchini inayowezesha mtu kukamilisha miamala ya kifedha bila matumizi ya Intaneti.
.

0 comments:

Post a Comment