Wednesday 19 September 2018

KAMPUNI YA VINYWAJI YA COCACOLA YAJIPANGA KUTENGENEZA KINYWAJI CHENYE BANGI


Kampuni hiyo maarufu ya kutengeza vinywaji vilaini ipo kwenye mazungumzo na Kampuni ya kutengeneza bangi, Aurora Cannabis ili kutengeneza kinywaji hicho
-
Inaelezwa kuwa lengo kuu la Kinywaji hicho kitakachotengenezwa na bangi aina ya cannabidiol litakuwa ni kupunguza maumivu(kutumika kama dawa) na si kulewesha
-
Aidha, Kampuni hiyo bado haijazungumza hadharani mpango huo lakini imekiri kwamba inafuatilia kwa karibu matukio katika sekta ya vinywaji vyenye bangi
-
Cannabidiol ni moja ya viungo vinavyopatikana ndani ya bangi na kinaweza kusaidia kupunguza kuvimba, maumivu na kuganda kwa misuli

0 comments:

Post a Comment