Wednesday 5 September 2018

Millard Ayo,Faraja Nyalandu,Ali Kiba,Samatta vijana wenye ushawishi Afrika



Majina 100 toka mataifa 26 ya Afrika yametajwa na mtandao wa Africa Youth Awards kwenye list ya mwaka 2018 ya vijana 100 wenye ushawishi mkubwa.

Kati ya hao 100, majina ya Watanzania 12 yametajwa pia: Ali Kiba, Millard Ayo, Mbwana Samatta, Faraja Nyalandu, Herieth Paul na wengine.

Huu ni mwaka wa tatu wa tuzo hizo mahususi kwa vijana kwenye nyanja kama: Siasa, Harakati, Ujasiriamali, Burudani, Washawishi wa mtandaoni na Wanamichezo ambao wanatangaza sura ya Afrika kwa muonekano chanya kwenye ramani ya dunia.

0 comments:

Post a Comment