Monday 10 September 2018

Serena Williams apigwa faini kwa utovu wa nidhamu


Mwanadada Serena Williams ametozwa faini ya fedha pauni za kiingereza 13,156 kutokana na makosa matatu tofauti aliyoyafanya kwenye mechi ya fainali ya michuano ya tennis ya Marekani uliopigwa siku ya jumamosi.
Kosa la kwanza ilikuwa ni kumtolea maneno ya dhihaka mwamuzi, kosa la pili kuzungumza mara kwa mara na mwalimu wake akiwa mchezoni na kosa la tatu ikiwa ni kuvunja kwa hasira raketi yake ya kuchezea.
Ikumbukwe kuwa kwenye mechi hiyo ya fainali kwa upande wa wanawake, Serena alifungwa na Naomi Osaka kutoka Japan, faini yake hiyo aliilipa kwa lazima kwa fedha hizo kukatwa kwenye malipo ya zawadi yake ya mshindi wa pili zipatazo pauni milioni 1.43.

0 comments:

Post a Comment