Mchezaji bora namba moja wa
zamani kwa upande wa wanawake, Serena Williams amefanikiwa kutinga robo
fainali ya mashindano ya US Open kwa ushindi wa seti (6-0, 4-6, 6-3).
Kaia Kanepi aliyetinga hatua hiyo bila kupoteza seti hata moja alishindwa kuhimili uwezo wa Williams licha ya kushinda kwenye seti ya pili kwa 6-4 hali iliyopelekea mchezo huo kwenda kwenye raundi ya tatu.
Serena aliyemtoa dada yake Venus kwenye raundi iliyopita hakusita kuonyesha furaha yake baada ya mchezo huo na kusema mpinzani wake alikuwa mchezaji hodari.
Mmarekani huyo atakutana na Karolina Pliskova kwenye robo fainali na iwapo atashinda huenda akakutana na bingwa wa zamani wa mashindano hayo Maria Sharapova ambaye pia ametinga robo fainali baada ya ushindi wa seti mbili mfululizo za 6-3, 6-2) dhidi ya Jelena Ostapenko.

0 comments:
Post a Comment