Monday 17 September 2018

UGANDA YAITAKA EU KUACHA KUINGILIA MASUALA YA AFRIKA


Kupitia msemaji wake Ofono Opondo yautaka Muunganiko huo wa Ulaya kutatua matatizo yake kwanza na kuacha kuingilia masuala ya bara la Afrika
-
Yasema haitakubali Umoja wa Ulaya kuishurutisha kufanya masuala yasiyouhusu na kuwa Uganda ina mifumo yake ya kujitawala
-
Aidha, imesema kuwa uhasama wake na EU ni kutokana na kushindwa kuidhinisha ndoa za jinsia moja na uhusiano wake na nchi ya China
-
Kauli hizo zinakuja ikiwa ni baada ya EU kuitaka Serikali ya Museveni kuheshimu haki, demokrasia na Mihimili mingine ya Serikali ikiwemo Bunge

0 comments:

Post a Comment