Thursday 30 November 2017

Ali Kiba aja na kibao kipya

Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa anatamba na kibao chake cha 'Seduce me' Alikiba ameamua kuachia video ya wimbo wake wa zamani ambao ulivuja kama zawadi kwa mashabiki wake katika siku yake ya kuzaliwa. 

Alikiba ambaye jana alikuwa anasherehekea kumbukumbu yake ya kuzaliwa aliamua kuachia video ya wimbo wa 'Maumivu Per Day' kama njia ya kusherekea siku hiyo na mashabiki zake.
"Nashukuru sana watu ambao wamenitakia kheri katika siku yangu ya kuzaliwa, nimejaliwa, kupendelewa na kupendwa pia nashukuru sana kwa jambo hilo, nawapenda wote na nitafanya kazi kwa nguvu zote kuwafanya mjivunie uwepo wangu. Maumivu Per Day ni kati ya nyimbo zangu za zamani zinazopendwa nimeamua kuitoa japo siyo rasmi ili kusherehekea kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa na mashabiki zangu" alisema Alikiba

0 comments:

Post a Comment