WAZIRI wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, amezindua huduma mpya itakayowawezesha
waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kutumia
mtandao wa Internet.
Mhe. Mhagama amezindua huduma hiyo leo Novemba
29, 2017, wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa
Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa, AICC, Arusha.“Huduma hii itawawezesha waajiri
kujisajili na Mfuko kupitia mtandao wa internet na hawalazimiki kujaza
fomu na kuja ofisini kwetu au kwa maafuisa kazi” Mkuu wa kitengo cha
Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, alisema wakati akitambulisha huduma
hiyo kwa Mhe. Waziri.
Katika hatua nyingine, Benki ya NMB Bank
plc imenyakua tuzo baada ya kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji
michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi.
Kampuni zingine
zilizonyakua tuzo kundi la waajiri ni Steel Master Ltd kwa kuwa mwajiri
bora katika uwasilishaji nyaraka za madai ya fidia kwa wafanyakazi na
kampuni nyingine ni KPMG Advisory Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika
uwasilishaji michango miongoni mwa kundi la waajiri wenye wafanyakazi
wengi.
WCF iliwatunukia tuzo wadau wa Mfuko huo ambapo Waziri Jenista
kwa niaba ya Serikali alipokea tuzo hiyo, kwa kutambua mchango wa
Serikali katika kuanzisha na kufanikisha utendaji wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi.
Wadau wengine ni Shirika la Vyama vya Wafanyakazi,
(ATE), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, (TUCTA), Mamlaka ya
Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), kwa kutambua ushiriki wake katika
uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF)

Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, akielezea jinsi huduma hiyo iyakavyofanya kazi.

WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu
wa WCF, Bw. Masha Mshjomba, wakishuhudia Mwenyekiyti wa Bodi ya
Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, (kushoto), akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya shilinhi milioni 15, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.
Mrisho Gambo, ikiwa ni mchango wa Mfuko kusaidia mpango wa elimu mkoani
humo. Makabidhiano haya yamekwenda sambamba na ufunguzi wa Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Wadau wa WCF jijini Arusha

Waziri
Mhagama (watatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.
Eric Shitindi, (wakwanza kushoro), wakipokea hundi yenye thamani ya
shilingi milioini 33.8 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
WCF, Bw. Emmanuel Humba, (wapili kushoto). Fedhab hizo ni kwa ajili ya
kusaidia ununuzi wa komputa nundu (perkins Braille Machines) kwa ajili
ya wanafunzi wenye ulemavu wa kuona katika shule za umma.

Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya WCF,. Wakwanza kushoto ni katibu wa Waziri Jenista Mhagama.

Mheshimiwa
Waziri Jenista Mhagama, akimkabidhi tuzo Bw. Richard L.Makungwa kutoka
NMB Bank Plc tuzo ya mwajiri mwajiri bora katika uwasilishaji michngo
miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini
ya WCF, Bw. Emmanuel Humba.
0 comments:
Post a Comment