Saturday 25 November 2017

Angela Merkel bado aongoza hana mpinzani


Ni kweli Angela Merkel anashindwa na mambo kadhaa, lakini bado anaongoza dhidi ya wanasiasa wengine nchini Ujerumani Angela Merkel anaendelea kuwa na sifa ya kuwa kansela bora zaidi wala hajatokea mpinzani
Miaka kumi na mbili iliyopita kansela Angela Merkel aliibuka kuwa kansela wa kwanza mwanamke nchini Ujerumani. Na hadi sasa kama kusingetokea matatizo katika kuunda serikali ya umoja baada ya kumalizika uchaguzi bibi Merkel angelikuwa ni kansela aliyechaguliwa kwa mara ya nne lakini baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja na vyama vingine bibi Merkel anakosa wingi wa viti ndani ya bunge la Ujerumani "Bundestag”.
Hali hii naweza kuonekana kana kwamba mgogoro unanukia au nguvu ya Merkel inapungua. Lakini wala haionyeshi hali kuwa imefikia mahala hapo hasa wakati bibi Merkel pale alipotembea ndani ya bunge, na kupena mikono na wabunge. Na mara alipomuona na kumpungia mkono Paul Ziemiak, mwenyekiti wa tawi la vijana la chama chake cha CDU na baadae wawili hao wakaketi pamoja nyuma ambako kulikuwa hakuna watu na wakafanya mazungumzo ya faragha.
Mwenyekiti wa tawi la vijana la CDU Paul Ziemiak
Ziemiak na wafuasi wake mara nyingi  katika siku zilizopita walikuwa wakimlaumu Kansela Angela Merkel lakini kwa sasa wanaonekana kuwa wamebadili mawazo yao na kuunga mkono kauli zinazoashiria kuwa bibi Merkel ndiye chaguo zuri katika kuiongoza nchi: anasema "Ujerumani inahitaji utulivu, na kama kuna mtu anayesimama  utulivu, basi mtu huyo ni Angela Merkel. "
Lakini  maneno hayo siyo waliyokuwa wakiyasema siku za hivi karibuni baada ya uchaguzi wa Septemba 24.Chama cha Christian Democtarac Union (CDU) pamoja na chama ndugu cha Christian Social Union (CSU) vyama hivyo vilipata asilimia 33 tu ya kura,hayo yakiwa ni matokeo yao mabaya kabisa tangu 1949.
Kansela Angela Merkel na vijana wa CDU (picture alliance/dpa/M. Skolimowska) Kansela Angela Merkel na vijana wa CDU
Kutokana na kitisho hicho cha kupoteza umaarufu tawi la vijana wa CDU lilisema kuwa chama hicho kimepoteza uaminifu wake. Vijana wa tawi la CDU walisema ahadi kuu katika uchaguzi ya muendelezo na utulivu, haitoweza tena kutekelezwa. Lakini Kansela haoni sababu yoyote ya kujilaumu kwa kushindwa kwenye uchaguzi.
Andreas Rinke, mwandishi wa habari na shirika la habari la Reuters ambaye yuko mjini Berlin mesema Merkel anaona mambo tofauti kabisa na taswira iliyopo, yaani kwa mtazamo wake anaona kuwa matokeo ya uchaguzi yalikuwa si mazuri lakini sio mabaya. mwandishi huyo amekuwa akifuatilia hatua za Merkel kwa miaka mingi na mnamo mwaka 2016 alitoa kitabu kinacho muhusu kansela Merkel : "Das Merkel-Lexikon: Die Kanzlerin von A-Z" yaani ufafanuzi wa Merkel kuhusu Ukansela kutoka A mpaka Z.
Katika kitabu hicho cha Rinke, neno "kushindwa" lina sehemu yake kwenye ukurasa na mwisho wake kuna mstari unaosema: "Kwa Merkel, kushindwa si sawa na kushindwa kabisa na wa mwisho."

0 comments:

Post a Comment