Thursday 23 November 2017

Kemikaze ajibu tuhuma juu ya kutuma picha zenye 'utata' za Feza Kessy

Msanii wa Bongo Fleva Cyril Kamikazeamejibu tuhuma zinazomuhusu juu ya kuanika picha za mpenzi wake Feza Kessy zikionesha sehemu ya mwili wake kupitia mtandao wa kijamii.
Kamikaze ameyasema hayo kupitia kipindi cha Enews kuwa haoni tatizo lolote la ile picha kwani ni picha  ya kawaida sana na haijaonyesha kiungo chochote cha Feza anachojua ni kwamba picha ile inaonyesha sehemu kidogo ya matiti  ya Feza ambapo ni sawa tu na wanawake wanaovaa brazia kuyabusti maziwa yao ili yaonekane.
Hata hivyo Kamikaze amesema hawezi kumdhalilisha Feza kwani anamuheshimu sana na Feza ndo alipiga ile picha na kumtumia yeye na hata alipoipenda na kuamua kuipost katika mtandao wake wa instagram alimpigia Feza kumuambia kuwa anaipost na Feza alikubali bila wasiwasi
Kamikaze amemalizia kwa kusema kuna wasanii wengi wanapiga picha za utupu zaidi hata ya ile mbona watu hawashangai?anamalizia kwa kusema watu wanapaswa kufahama kwamba Feza ni msanii na anapaswa kupiga picha za aina ile ilimradi hayupo uchi.
 

0 comments:

Post a Comment