Pablo Picasso
Umuhimu wa Picasso
Picasso anahesabiwa kati ya wasanii wakuu wa karne ya 20. Alibadilisha uzoefu jinsi ya kuona dunia katika utamaduni wa Kimagaharibi wa Ulaya na Marekani. Mtindo wake wa uchoraji ulianza kutumia maumbo ya jiometria. Katika hatua hii aliathiwirwa na sanaa ya Afrika.
Kipindi cha buluu: Picha ya Suzanne Bloch (1904)
Mwanzo wa kazi
Picasso alianza kuchora kwa umri mdogo wa miaka saba akisaidiwa na babake aliyekuwa mwalimu wa sanaa. Akiwa na miaka 10 aliandikishwa kwenye chuo cha sanaa na 1895 alipokelewa kwenye chuo kikuu cha sanaa huko Barcelona.Alitembelea sana makumbusho penye taswira na sanamu za wasanii waliotangulia. Alipenda kusafiri penye maonyesho makubwa kama Madrid au Paris.
Taswira zake za awali badi zililingana zaidi na picha jinsi zilivyokuwa kawaida. Mwanzoni alipenda rangi ya buluu na mfano wake ni picha ya Suzanne Bloch hapo chini.
Baada ya kuona sanaa ya Afrika: Mabinti wa Avignon (1910)
Athira ya Kiafrika na mtindo mpya
Mjini Paris alikuta maonyesho ya sanaa ya Kiafrika iliyomwathiri sana. Hii inaonekana katika "Mabinti wa Avignon" (1910).Baadaye aliendelea kuvunja maumbile ya kawaida na kuyajenga upya kwa kutumia maumbo ya kijiometria. Mtindo huu uliitwa "cubisme" kwa Kifaransa yaani "umchemraba" kutokana na mchemraba kama umbo la kijiometria linalotumiwa kujenga upya maumbile ya yale yanayoonyeshwa kwenye picha.
Ukubisti (uchembemraba): Picha ya Juan Gris (1912)
Kwa jumla imekadiriwa ya kwamba Picasso aliumba kazi za sanaa zaidi ya 20,000 kama vile taswira, picha za mchapo na sanamu.
Maisha ya binafsi
Picasso alioa mara mbili lakini alikuwa na wapenzi wengi. Alizaa watoto wanne na wake watatu.
"Guernica" (1937) imechorwa baada ya kuangamizwa kwa mji wa Guernica
Tangu 1961 aliishi katika Ufaransa ya Kusini alipoaga dunia 1973. Aliacha taswira maelfu ya akiacha
0 comments:
Post a Comment