Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amedai
kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na msajili wa
vyama Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni Profesa wa ajabu ambaye anaweza
kubomoa chama alichokijenga.
Akiwa
kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Mtwara, Mh. Mbowe amesema kwamba hana
ugomvi wowote na Prof Lipumba ingawa amekiri atakuwa muongo akisema
kwamba anamuheshimu kwani anatumika katika kukivuruga chama alichokuwa
akikiongoza kwa muda mrefu.
Mh.
Mbowe amesema kwamba wakati CUF ikishirikiana na UKAWA kwa ujumla
kutafuta kura na kuongeza wabunge wa chama hicho bungeni, yeye Prof
Lipumba alikuwa mafichoni na anamshanga sasa hivi anavyorudi ndani ya
chama hicho na kutaka kukisambaratisha.
"Sina
ugomvi na Prof Lipumba lakini nikisema namuheshimu nitakuwa muongo
sana. Prof Lipumba ni msomi sana tena msimchezee kwenye elimu lakini
usomi ni jinsi unavyotumia elimu yako lakini siyo wingi wa vyeti. Ni
Profesa wa ajabu kweli kweli. Mimi simuogopi mtu nitazungumza straight.
Amesema Mbowe
Pamoja
na hayo Mbowe amedai kwamba Spika wa Bunge pamoja na Msajili wa vyama
vya siasa wanatumika katika kuibomoa CUF na kuongeza kwamba hataacha
kusema ukweli kwani hakuna mtu yoyote anayemuogopa isipokuwa Mungu
pekee.
Ameongeza
kwamba kasi inayotumika kuibomoa CUF inatumika pia kuibomoa CHADEMA na
kuweka wazi kwamaba siku chama cha Chadema kikiuliwa labda awe amefariki
lakini siyo wakati huu ambao bado anapumzi.
0 comments:
Post a Comment