Bahari ya Mediterania ni njia hatari zaidi duniani kwa
wahamiaji wanaofanya juhudi za kufika barani Ulaya-lasema shirika la
uhamiaji la UN
Zaidi ya watu 33,000 wamefariki wakijaribu kufanikisha safari hatari
kabisa ya kuvuka bahari ya Meditterania tangu mwaka 2000 kwa mujibu wa
ripoti za Umoja wa Mataifa.Wakati njia kati ya Uturuki na Ulaya ikiwa
imefungwa shinikizo linazidi kuongezeka katika njia nyingine ya kuelekea
Itali.Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema Ijumaa
kwamba bahari ya Meditterania imebakia kuwa ndio kivuko hatari kabisa
kinachoangamiza uhai wa watu wengi duniani huku zaidi ya wakimbizi
33,000 wakifariki wakijaribu kuvuka kwa njia hatari kupitia bahari hiyo
tangu mwaka 2000.Hatari yaongezeka
Ijapokuwa idadi ya vifo imepungua tangu iliposhuhudiwa rekodi kubwa ya watu wanaowasili katika ardhi ya Ulaya tangu mwaka 2014 hadi 2016,hatari au kitisho cha kutokea vifo wakati wa safari hiyo kimeongezeka kwa kiwango kikubwa kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa na shirika la IOM.
Mtaalamu huyo anasema kuifunga njia fupi iliyokuwa ikitumiwa mwanzo na wahamiaji ambayo sio hatari sana ni hatua inayoweza kufungua njia nyingine ndefu na zilizo hatari zaidi na hivyo basi kuongeza uwezekano wa watu wengi kupoteza maisha baharini.
Kadhalika anasema ushirikiano kati ya Ulaya na Uturuki wa kuzuia wimbi la wakimbizi sasa unafinikwa na Libya ambayo ni kituo kikuu hivi sasa cha wahamiaji wanaosubiri kuvukishwa kwa njia za magendo kuingia Ulaya.Hata hivyo mwelekeo huo sio tu haufai lakini pia kuna uwezekano mkubwa wa kutofanikiwa kwa kuangalia ule ukweli kwamba Libya inakabiliwa na utawala mbaya ,ukosefu wa usalama na mgawanyiko wa kisiasa.
Wakimbizi wa kiuchumi waongezeka
Zaidi ya wahamiaji 161 na wakimbizi wamewasaili Ulaya mwaka huu huku asilimia 75 ya wakimbizi hao wakiwasili Itali kupitia njia ya kati ya bahari ya Mediterania.Mwaka 2015 Umoja wa Ulaya ulishuhudia ongezeko kubwa kabisa la wahamiaji katika nchi hizo wengi wao wakiwa wamekimbia vita mashariki ya Kati,Asia na Afrika ambapo Ujerumani ilipokea kiasi watu 900,000.
Hata hivyo serikali zinasema kwamba chini ya thuluthi moja ya wahamiaji waliowasili Itali mwaka huu wanatafuta hifadhi ikitajwa kwamba ni wakimbizi wa kiuchumi.Wengi walioingia Ulaya mwaka huu wametokea Nigeria,Eritrea na Guinea.
0 comments:
Post a Comment