Wednesday 8 November 2017

Mfumuko wa bei wa taifa umeshuka



Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia  Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Irenius Ruyobya imetangaza kushuka kwa mfumuko wa bei nchini kutoka asilimia 5.3 hadi 5.1.
Mfumuko wa bei wa taifa umeshuka kwa mwezi Oktoba, ikilinganishwa na ilivyokuwa mwezi Septemba. Bw. Ruyobya ameeleza kuwa hiyo ina maana kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2017 imepungua ikilinganishwa na ilivyokuwa kipindi kama hicho mwaka jana.
Ruyobya ameongeza kuwa kupungua huko kwa mfumko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba mwaka huu.
Aidha, Ruyobya amebainisha kuwa mfumko wa bei nchini unakaribiana na nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya mfumko wa bei umepungua hadi asilimia 5.72 kutoka asilimia 7.06 huku nchini Uganda umepungua hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.3 kati ya mwezi Septemba na Oktoba.

0 comments:

Post a Comment