Thursday 2 November 2017

Mwanafunzi auwa mwalimu wake darasani na kutuma mitandaoni


Mwanafunzi mmoja wa Chuo cha Moscow Polytechnic College  nchini Urusi amemuua mwalimu wake mapema baada ya muda wa mapumziko.


Mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina la Andrey Emelyanenkov (19) alichukua maamuzi hayo baada ya mfululizo wa kupewa adhabu na mwalimu huyo kwa makosa ya utovu wa nidhamu chuoni hapo ikiwemo kufeli somo lake la Usalama na Ulinzi wa Jamii.

Mwalimu huyo aliyeuawa ametambulika kwa jina la Sergey Danilov inaelezwa kuwa alibaki darasani na kijana huyo wakati wanafunzi wengine wakiwa nje kwa mapumziko mafupi ya kifungua kinywa.
Baada ya kutekeleza mauaji hayo, Emelyanenkov alichukua simu yake na kupiga selfie na mwili wa marehemu uliokuwa umedondoka sakafuni kisha kusambaza picha hizo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi alichukua msumeno wa moto (Chainsaw) na kujiua kwa kujikata koromeo.
Wanafunzi wenzake wameeleza kuwa Emelyanenkov alibakia darasani kwa mahojiano na mwalimu huyo baada ya kufanya vibaya kwenye somo lake na makosa mengine ya kinidhamu.
Tayari polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea jana (Jumatano) asubuhi baada ya kutokea kwa vurugu kati yao na kudai kuwa bado upelelezi wa kina unaendelea.
Leo (Jana jumatano) katika chuo kimoja hapa Moscow tumekuta miili ya watu wawili wakiwa wamefariki mmoja amezaliwa mwaka 1979 na mwingine mwaka 1999 na mwili wa mmoja ulikuwa umechomwa chomwa na kisu na mwingine akiwa amejikata shindoni na kitu chenye makali, Bado uchunguzi wa kina unaendelea.“amesema afisa upelelezi wa Jeshi la polisi mjini Moscow, Yulia Ivanova kwenye ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Habari la Interfax la nchini Urusi.
Polisi wamesema walikuta video kwenye simu yake ikiwaonesha wawili hao wakigombezana na baadhi ya picha za Mwalimu huyo akiwa amelala sakafuni zikiwa zimepigwa na kutumwa kwenye makundi ya WhatsApp.

0 comments:

Post a Comment