Thursday 9 November 2017

Rais wa Gabon ajiandaa kuandaa albamu na msanii nchini kwake


 Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba anafanya kazi ya kuandaa albamu akishirikiana na msanii mkongwe wa nchi hiyo Frederic Gassita.
Akithibitisha habari hizi msanii kutoka Tanzania Vanessa Mdee na mtangazaji wa Kings FM ya Njombe, Gami Dee amesema, “Frederic ni msanii ambaye anashirikiana sana na Rais wa Gabon Mhe. Ondimba. Yeye na Frederic wanafanya project ya pamoja inaitwa The African Queens Project, kwenye hiyo project albamu nzima ambayo itawashirikisha wasanii wa kike wa Kiafrika.”
Malkia huyo wa muziki wa Bongo Flava ameongeza kuwa wimbo wa Imara ambao ameshirikishwa na Gassitta ni ngoma ambayo itakuwa ya kwanza katika albamu hiyo inayotayarishwa.

0 comments:

Post a Comment