Thursday 9 November 2017

Serikali yaiomba Mahakama kumuongezea miaka 15 mwanariadha Pistorious



Serikali ya Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya juu nchini humo kumwongezea kifungo mwanaridha mlemavu, Oscar Pistorius ‘Blade Runner’ aliyekutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp, Februari 2013.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Pretoria, Thokozile Masipa, alimhukumu Pistorius kifungo cha miaka sita baada ya kumtia hatiani kwa mauaji ya bila kukusudia, uamuzi ambao haujawaridhisha watu wengi.
Hivi karibuni, serikali hiyo kupitia Wakili, Andrea Johnson, ilirejea mahakamani na kuomba uamuzi wa Jaji Masipa ubatilishwe na mwanaridha huyo aliyejipatia umaarufu kwa kushiriki mbio akitumia miguu ya bandia kwa kuwa ni mlemavu, aongezewa muda zaidi wa kukaa jela.
“Jaji aliyeisikiliza kesi alikosa kabisa kuweka wazi sababu za kutotoa adhabu ya kifungo kisichopungua miaka 15 (Kwa mujibu wa sheria za Afrika Kusini) alipomhukumu Oscar Pistorious kwa mauaji ya Reeva Steenkamp,” wakili huyo aliiambia mahakama hiyo ambayo bado inaisikiliza rufaa hiyo.

0 comments:

Post a Comment