Jitihada kubwa za uokoaji zinaendelea baada ya tetemeko kubwa kukumba eneo la mpaka wa Iran na Iraq na kuwaua zaidi ya watu 400 na kuwajeruhi zaidi ya 7,000.
Makundi ya uokoaji yanatafuta manusura waliokwamwa ndani ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Tetemeko hilo la ardhi ndilo baya zaidi kutokea duniani mwaka huu.
Watu wengine walioawa walikuwa kwenye mji ulio magharibu mwa Iran wa Sarpol-e-Zahab ulio umbali wa kilomita 15 kutoka mpaka na sehemu zingine za mkoa wa Kermanshah.
Hospitali kuu wa mkoa huo iliharibiwa vibaya na kusababisha ikubwe na matatizo ya kuwahudumia wagonjwa.
Mwanamke mmoja na mtoto waliondolewa kutoka kwa vifusi wakiwa hai kwenye mji huo, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Iran.
Majengo mengi katika mji huo yanaonekana kuporomoka.
0 comments:
Post a Comment