Monday 6 November 2017

Watu 26 wauwawa kwa kupigwa risasi Marekani wakiwa kanisani


Watu 26 wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wakiwa katika ibada ndani ya kanisa moja jimbo la Texas nchini Marekani.
Shambulizi  hilo limetokea katika kanisa la  First Baptist Church katika mji wa Sutherland Springs, mji mdogo katika wilaya ya Wilson, Texas.
Mshambuliaji, ambaye anadaiwa kuuawa baada ya kutekeleza mauaji hayo, aliingia kanisani na kuanza kuwafyatulia risasi watu mwendo wa saa tano unusu asubuhi (17:30 GMT).
Gavana Greg Abbott amethibitisha idadi ya waliofariki na kusema ndicho kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya texas.
"Kutakuwa na majonzi na masikitiko mengi kwa wale walioathiriwa," aliambia wanahabari.
Mkuu wa idara ya usalama wa Texas Freeman Martin amesema waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 5 na 72.
Maafisa wamesema watu zaidi ya 20 pia walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini.
Bw Martin amesema mshukiwa ni mwanamume mzungu wa umri wa miaka 20 ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi na fulana ya kujikinga dhidi ya risasi pamoja na kuwa na bunduki yenye uwezo mkubwa.
Alianza kufyatua risasi nje ya kanisa kabla ya kuingia ndani na kuendelea kufyatulia watu risasi.
A woman and her children take part in a vigil for victims of a mass shooting in Sutherland Springs, Texas, US., November 5, 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwanamke na watoto wake wakishiriki ibada ya mkesha kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio la Sutherland Spring, Texas
Wakazi walihudhuria mkesha wa kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio hilo la Sutherland SpringsHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWakazi walihudhuria mkesha wa kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio hilo la Sutherland Springs
Mwenyeji "alitwaa bunduki yake na kuanza kumfyatulia " risasi mshukiwa kabla ya mshukiwa huyo kutoroka akitumia gari.
Raia huyo alimwandama mshukiwa huyo ambaye aliendesha gari lake na kisha kuliangusha katika barabara wilaya ya Guadalupe.
Polisi waelimpata mshukiwa akiwa amefariki ndani ya gari lake.
Haijabainika iwapo alifariki kutokana na majeraha ya risasi aliyojisababishia mwenyewe au kutokana na mejaraha kutoka kwa raia huyo, Martin ameongeza.
FBI officials arrive at the site of a mass shooting in Sutherland Springs, TexasHaki miliki ya pichaKSAT 12 / REUTERS
Image captionFBI wamefika kufanya uchunguzi
Mshukiwa ametajwa kuwa Devin P Kelley, 26, kwa mujibu wa vyombo vya jhabari Marekani.
Polisi bado hawajathibitisha jina lake.
Mhubiri wa kanisa hilo la First Baptist Frank Pomeroy, ameambia ABC News kwamba binti yake wa miaka 14 kwa jina Annabelle ni miongoni mwa waliouawa.
Sutherland Springs ni mtaa mdogo wenye wakazi wasiozidi elfu moja ambao hupatikana kilomita 50 hivi kusini mashariki mwa mji wa San Antonio mjini Texas.
Maafisa wa FBI kutoka San Antonio wametumwa kufanya uchunguzi lakini kufikia sasa lengo la mshambuliaji halijabainika.
Map of Sutherland Springs AreaFBI pia wamesema mshambuliaji alikuwa mmoja pekee, lakini bado wanachunguza uwezekano wa iwapo kuna mtu mwingine aliyehusika.
Rais Donald Trump, ambaye yumo ziarani Asia, ameshutumu kisa hicho na kusema ni "kitendo cha uovu" na kusema kwamba Wamarekani watajikwamua na kusalia na umoja.
"Na kupitia kwa machozi na kupitia huzuni hii, tunasalia imara, imara zaidi," ameongeza.
Mauaji hayo yametokea mwezi mmoja tu baada ya mshambuliaji mwingine kufyatulia risasi watu waliokuwa wakihudhuria tamasha ya muziki Las Vegas na kuwaua watu 58 pamoja na kujeruhi mamia wengine, katika kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutumia bunduki katika historia ya Marekani nyakati za karibuni.

0 comments:

Post a Comment