Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Joseph Lebulu amejiuzuru katika
nafasi yake hiyo leo baada ya Baba Mtakatifu Francis kukubali ombi
lililowasilishwa kwake.
Katibu
mkuu wa TEC, Raymond Saba amethibitisha na kusema kuwa Papa Francis
amemteua Askofu Isaac Massawe wa Jimbo Katoliki Moshi, kuwa Askofu Mkuu
mpya wa Jimbo Kuu la Arusha.
Kwa mujibu wa redio Vatican, Askofu Mkuu mteule Massawe alizaliwa Juni 10, 1951 huko Mango, Jimbo Katoliki la Moshi.
Alipata
upadri Juni 29,1975 na Novemba 21, 2007 aliteuliwa na Baba Mtakatifu
mstaafu Benedict XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi na aliwekwa
wakfu Februari 22,2008 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo
Kuu la Dar es Salaam akisaidiana na Askofu Mkuu Lebulu na Askofu
Amedeus Msarikie (sasa marehemu) wa Jimbo Katoliki la Moshi. Hivi
karibuni, aliteuliwa kuwa msimamizi wa kitume Jimbo Katoliki la Mbulu.
0 comments:
Post a Comment