Thursday 28 December 2017

Russia yaitaka Marekani kutokuongeza mvutano kwenye peninsula ya Korea



Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov jana ameongea na mwenzake wa Marekani Bw. Rex Tillerson kwa njia ya simu na kusema, Marekani hairuhusiwi kuongeza hali ya hatari kwenye peninsula ya Korea kwa kauli za uchochezi na kuongeza jeshi lake kwenye peninsula hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema, pande hizo mbili zinaamini kuwa maendeleo ya makombora ya nyuklia ya Korea Kaskazini yamevunja azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kusisitiza kuwa inapaswa kuanzisha mchakato wa mazungumzo ya amani haraka iwezekanavyo.

0 comments:

Post a Comment