Klabu ya Atletico Madrid imedhamiria kwenda kuishtaki timu ya Barcelona shirikisho la soka Dunian FIFA kwakosa la kufanya ushawishi kwa kiungo msambuliaji wa timu yao Mfaransa Antonio Griezmann ili ajiunge na timu yao jambo ambalo ni kinyume na taratbu za Atletico Madrid.
Atletico Madrid wanaamini kuwa mazungumzo ya kinyume na sheria kati ya FC Barcelona na Antoine Griezmann yamefanyika, kitu ambacho hawawezi kukifumbia macho na watalifikisha suala hilo katika ngazi za juu za shirikisho la soka ulimwenguni FIFA. Antoine Griezmann alisaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Atletico Madrid mwezi Juni mwaka huu lakini amekuwa akihusishwa kuwa katika mipango ya FC Barcelona kwa zaidi ya wiki kadhaa sasa.

0 comments:
Post a Comment