Wednesday, 20 December 2017

Conte aogopeshwa na jambo la Djik kwenda Manchester City,adai itakuwa timu hatarishi



Conte ametishwa na suala la mlinzi wa klabu ya Southampton Virgil Van Djik kwenda kujiunga na Manchester City na anaamini kama jambo hilo litatokea basi itakuwa ngumu kwa wapinzani wa Man City kushindana nao na itawaumiza wengi.
Antonio Conte ameviambia vilabu vingine kwamba kama City wakichukua kila mchezaji bora itakuwa ngumu kuwazuia, Conte amesisitiza kwamba vilabu vingine vijaribu kuwapa City upinzani kwa Djik.
Djik alikuwa benchi katika mchezo kati ya Chelsea na Southampton mwishoni mwa wiki iliyopita na tayari kocha wa Southampton Maurcio Pellegrino amethibitisha kwa Djik anaweza kuondoka January.

0 comments:

Post a Comment