Tuzo za Dubai Global Soccer 2017 zilifanyika jana usiku huko Dubai na
kushuhudia nyota mbalimbali wakiibuka kidedea kwa kutwaa tuzo hizo kwa
mwaka 2017, nyota wa soka wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno
Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka. Wengine
walioshinda tuzo hizo ni kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ambaye
ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka 2017 wakati staa wa zamani wa AS
Roma Francesco Totti akishinda tuzo ya heshima. Wengine walioshinda tuzo
za Dubai Global Soccer Awards 2017 ni pamoja na Jorge Mendes wakala
bora 2017, Carlos Puyol tuzo ya heshima 2017, Felix Brych refa bora wa
mwaka 2017, Real Madrid wameshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka 2017 na
tuzo ya kocha bora wa timu ya taifa imeenda kwa kocha wa Misri Hector
Cuper.
0 comments:
Post a Comment