Tuesday, 19 December 2017

El clasico itawakutanisha tena vibonde Hispania

Baada ya kushinda fainali ya 5 ndani ya mwaka 2017 dhidi ya Gremio jumamosi iliyopita – jumamosi hii Real Madrid watacheza fainali ya mwisho ya mwaka 2017 dhidi ya Barcelona. Pamoja na kwamba huu umekuwa mwaka wa mafanikio kwa Real Madrid – wakishinda fainali 5 walizocheza mwaka 2017, huku mwaka ukiwa unaelekea ukingoni Madrid wamebakiza fainali moja. Katika mechi ya The Clasico dhidi ya Barcelona itakayopigwa December 23 – Los Blancos wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na pointi 11 nyuma ya mahasimu wao, ingawa wana mchezo mmoja mkononi.

Ushindi wa nyumbani kwa Zinedine Zidane utawarudisha Madrid katika mbio za ubingwa, matokeo mengine yoyote ya tofauti yatakuwa yanamaanisha mlima mrefu zaidi wa kuupanda katika kutetea taji lao la Laliga
Baada ya kushinda makombe 5 mwaka 2017 wanahitaji kushinda mchezo wa jumamosi hii ili kuweka hai ndoto za kuongeza taji la sita miezi mitano ijayo. Kwa mara ya kwanza Zidane atakuwa na kikosi chake chote katika mchezo wa La Liga ndani ya msimu huu. Lakini wanaumana na Barcelona ambayo imeimarika na yenye rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja msimu huu kwenye La Liga.

0 comments:

Post a Comment