Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis (MB)
anayekabiliwa na makosa ya rushwa ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya
Hakimu Mkazi Dodoma.
Sadifa
amefikishwa mahakamani leo Jumanne Desemba 19,2017 baada ya kukosa
dhamana Jumatatu Desemba 11,2017 kutokana na upande wa mashtaka
kuwasilisha hati ya kiapo kuzuia dhamana kwa madai kuwa angevuruga
upelelezi na kuingilia uchaguzi wa UVCCM uliofanyika Desemba 10 na
11,2017 mjini Dodoma.
Mahakama
leo imetupilia mbali pingamizi hilo na kutoa masharti ya dhamana kwamba
Sadifa awe na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh1 milioni na
wenye vitambulisho vinavyotambuliwa na mamlaka ya maeneo wanakoishi.
Sadifa
pia ametakiwa kutotoka nje ya mipaka ya nchi bila kibali cha Mahakama.
Amekidhi masharti hayo na amechiwa kwa dhamana na kesi itatajwa Januari
18,2018.
Alipofikishwa
mahakamani awali, wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Biswalo Biswalo alidai Sadifa anashtakiwa kwa makosa mawili.
Katika
shtaka la kwanza anadaiwa Desemba 9,2017 katika makazi yake kwenye Kata
ya Mnada mjini Dodoma akiwa mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM aliwahonga
wanachama ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya
makamu mwenyekiti katika uchaguzi mkuu wa umoja huo.
Sadifa
katika shtaka la pili anadaiwa katika eneo hilo na siku hiyohiyo,
aliwaahidi kuwalipia usafiri wanachama wa umoja huo kuwasafirisha kutoka
Dodoma hadi Kagera kama zawadi ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa
akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi huo.
Biswalo
alisoma hati ya kiapo iliyotolewa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa
Dodoma, Emma Kuhanga kupinga maombi ya dhamana kwa sababu endapo atapewa
dhamana atavuruga upelelezi na kuingilia uchaguzi wa vijana.
Wakili
wa Utetezi, Godfrey Wasonga alipinga hoja hiyo akisema makosa
aliyoshtakiwa nayo mteja wake yana dhamana na hawezi kuingilia uchaguzi
kwa kuwa ulishafanyika na mshindi alishatangazwa.
Kutokana
na mabishano hayo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma,
Joseph Fovo aliahirisha kesi hadi leo Desemba 19,2017 kutoa nafasi ya
mahakama kupitia kiapo kilicholetwa na upande wa mashtaka ili kutoa haki
katika maombi ya dhamana ya mshtakiwa. Sadifa alipelekwa rumande.

0 comments:
Post a Comment