Wednesday 27 December 2017

Harry Kane aweka rekodi mpya ya mwaka

 

Harry Kane amefunga hat-trick na hivyo kumfanya kuweka rekodi mpya ya mabao mengi yaliofungwa kwa mwaka huku Tottenham ikiicharaza Southampton katika uwanja wa Wembley.

Mshambuliaji huyo wa Spurs na Uingereza alifunga bao lake la 37 la mwaka 2017 katika dakika ya 22 na hivyobasi kuipiku rekodi ya Alan Shearer aliyoweka wakati alipokuwa akiichezea Blackburn 1995.
Kane baadaye aliongeza mabao mengine mawili katika vipindi vyote viwili na kufanya jumla ya mbao aliyofunga kwa klabu na taifa kuwa 56 mawili zaidi ya mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi.

0 comments:

Post a Comment