Saturday 9 December 2017

Kampuni ya Unilever yainua mradi wa chai Rwanda


Kampuni ya Unilever imezindua mradi wa chai wa dola milioni 30 katika wilaya ya Nyaruguru nchini Rwanda. Unilever ni mojawepo wa kampuni kubwa za kimataifa inayouza bidhaa za chakula na za matumizi ya nyumbani wa zaidi ya nchi 190.
Mradi huo unaanzishwa mwaka mmmoja baada ya serikali kusaini makubaliano na kampuni hiyo kuwekeza dola milioni 30 ndani ya miaka minne ijayo katika miradi ya chai.
Zaidi ya ekari 3,500 zitapandwa chai chini ta mradi huo na kufungua nafasi 1,000 za ajira.
Waziri wa kilimo Gerardine Mukeshimana amewaambia maelfu ya wakulima wa chai kujinufaisha na uwekezaji huo ili kuinua hali yao ya maisha.

0 comments:

Post a Comment