Thursday 28 December 2017

Kiongozi kamati ya maandalizi Kombe la Dunia 2018 ajiuzuru


Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maandalizi ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 nchini Urusi, Vitaly Mutko amejiondoa katika nafasi hiyo kutokana na mvutano uliojitokeza kati yake na kamati ya kimataifa ya olimpiki kuhusu program ya kupima matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni miongoni mwa wachezaji wa Urusi.
Licha ya kung'atuka Mutko ambaye ni naibu waziri mkuu ambaye ndiye kiongozi mkuu wa chama cha mpira wa miguu nchini Urusi, alikuwa tayari amekamilisha maandalizi ya viwanja akiwa kiongozi wa kamati.
Kufuatia kujiuzulu kwake, majukumu ya kamati hiyo yanabaki mikononi mwa makamu wake ambaye ataiongoza hadi wakati wa mashindano Bw. Alexey Sorokin.

0 comments:

Post a Comment