Tuesday, 19 December 2017

Kampuni tafiti yaitaka Kenya kupunguza hasara katika chakula ili kudhibiti njaa

Ripoti iliyotolewa na watafiti kutoka jopo la washauri la Chuo cha Tegemeo nchini Kenya imesema, nchi hiyo inatakiwa kuongeza uwekezaji kwenye maghala ya kisasa, mfumo mzuri wa usafiri na elimu kwa wakulima ili kupunguza hasara inayotokea baada ya mavuno.

Watafiti hao wamesema, Kenya ni moja ya nchi zenye kiwango cha juu cha uharibifu baada ya mavuno ya mahindi, ambao unazuia juhudi za nchi hiyo kuwapatia chakula watu wake. Wamesema hasara hiyo inachangia pakubwa katika upungufu wa chakula na lazima ikabiliwe ipasavyo kama mkakati wa kutimiza lengo la usalama wa chakula.
Utafiti huo umebaini kuwa uharibifu mkubwa baada ya mavuno ya mahindi nchini Kenya unatokana na ukosefu wa maghala ya kisasa na mabadiliko ya hali ya hewa.

0 comments:

Post a Comment