Sunday 10 December 2017

Kocha mkuu Kili Stars 'kukata tamaa kwangu mwiko'



Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje amesema “always next time”, akimaanisha wakati mwingine baada ya Stars kushindwa kufanya vizuri katika michuano hiyo.
Wakati akihojiwa, Ninje alionekana ni mchangamfu, akisifia vijana wake walivyocheza na kuongeza kwamba “until next time”.
Kili Stars inafungwa mechi ya pili mfululizo baada ya kuwa imelala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Zanzibar Heroes ambao walianza kwa kufungwa, wakasawazisha na kupata ushindi.
Wapenda soka wengi nchini wameonekana kukerwa na kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoshiriki michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Hata hivyo, Mashabiki wa soka wamekuwa wakijadili uwezo wake na baadhi wanaeleza kwamba Uingereza alifundisha timu za watoto na hakuwa na nafasi ya kufundisha timu ya taifa.
Kill Stars ilifungwa mabao 2-1 na Rwanda ikiwa imetangulia kufunga na baadaye Amavubi wakasawazisha na kupata bao la ushindi.

0 comments:

Post a Comment