Tuesday 26 December 2017

Mechi za leo ligi kuu Uingereza


Leo 26, Disemba zinachezwa mechi maalum za  ligi kuu katika siku maalum ya sikukuu maarufu kama Boxing Day Special ambapo mechi hufanyika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea.
Leo kutapigwa mechi nane pekee, na kutokana na sababu za kiitifaki, mechi moja nyinge itapigwa kesho na nyingine moja.
Mechi hizo, Tottenham Hotspurs watashuka dimbani kuchiza na Southampton, Man United dhidi ya Burnley, Watford watacheza na Lceister City na Huddersfield watawakaribisha Stoke City katika uwanja wa John Smith.
AFC Bournemouth watakuwa wenyeji wa West Ham United, Chelsea dhidi ya Brighton, wakati West Brom watawaalika Everton na Liverpool watakuwa nyumbani Anfield kucheza na Swansea City.
Vinara wa Ligi hiyo Manchester City watakuwa ugenini kesho kucheza dhidi ya Newcastle united, na mechi nyingine itakuwa keshokutwa ambapo Arsenal watacheza na Crystal Palace.

0 comments:

Post a Comment