Tuesday, 19 December 2017

Mkuu wa walinda amani wa UN akutana na Rais wa Congo


Siku chache baada ya walinda amani 14 kutoka Tanzania kuuawa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mkuu wa walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa amekutana na Rais Joseph Kabila
Kongo Friedenswächter ermordet (picture-alliance/AP Photo/J. Delay) Walinzi wa amani wa UN, wakilinda katika eneo la Goma, DRC. Waasi walishambulia walinda amani na kuwaua 14 mnamo Desemba 7.
Jean Pierre Lacroix  alifanya mazungumzo na Rais Kabila jana, ambapo waliangazia usalama na uchaguzi mpya nchini humo.Awali, Lacroix alitembelea mji wa Goma siku ya Ijumaa, na kuwaangalia walinda amani 30 waliojeruhiwa katika shambulio lililotokea katika mji wa Kivu Kaskazini, mnamo Desemba 7 mwaka huu.
Chanzo kimoja cha habari kilicho karibu na majeshi ya kulinda amani nchini Congo, MONUSCO, kimeliambia shirika la habari la AFP kuwa Kabila na Lacroix  walijadili kuhusu shambulio hilo, ambalo ni baya kabisa katika historia ya karibuni ya majeshi hayo.
Lacroix alisema machafuko katika upande wa mashariki wa Congo ni mrundikano wa matatizo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa pamoja. "Ushirikiano na nchi jirani ni muhimu sana," amenukuliwa Lacroix akizungumza kwenye Redio ya Umoja wa Mataifa.
Eneo kubwa la mashariki mwa Congo, limekabiliwa na machafuko kwa muda mrefu, lakini mapigano baina ya majeshi ya serikali na makundi ya wanamgambo, pamoja na mapambano ya kikabila yameongezeka zaidi mwaka huu.
Jimbo la Kivu Kaskazini, ambalo lipo mpakani mwa Uganda na Rwanda, limekabiliwa na mauaji  kwa kiasi kikubwa na utekaji nyara baina ya makundi ya waasi na ya kikabila.

0 comments:

Post a Comment