Tuesday, 19 December 2017

Mvutano waibuka kumchagua spika Bunge la Afrika Mashariki

Mvutano mkubwa uliibuka Jumatatu mjini Arusha, Tanzania, kuhusu ni wajumbe wa nchi zipi waliofaa kusimama ili kuchaguliwa kama spika wa bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mgogoro huo ulizuka pale Tanzania, Burundi na Rwanda ziliposimamisha wajumbe wao huku nchi zingine wanachama wa jumuiya hiyo zikipinga hatua hiyo.
Baadhi ya wajumbe walisema kwamba baadhi ya nchi zilizotaka kusimamisha spika hazikuwa na nia njema kwa sababu wajumbe wao walikuwa wamehudumu kama spika katika mabunge ya zamani na hivyo basi ilikuwa ni zamu ya nchi zingine kuwasimamisha wajumbe wao.

0 comments:

Post a Comment