Wednesday 27 December 2017

Mourinho ajitetea juu ya usajili

 

Kocha mkuu wa Manchester United Jose Mourinho adai kuwa tofauti yake na klabu ya Manchester City wamwekeza pesa nyingi sana na wanatumia pesa kubwa sana kununua wachezaji na ndio sababu timu yao imekuwa bora zaidi.

Toka Jose Mourinho akabidhiwe Manchester United amefanya manunuzi makubwa sana ikiwemo kuvunja rekodi ya usajili United kwa Pogba £89m, lakini pia kwa mshambuliajia wa Ubelgiji Romelu Lukaku £75m.
Kwa ujumla toka Mourinho apewe Manchester United mwezi May mwaka 2016 hadi sasa ameshatumia kiasi cha £300m lakini kocha huyo amesema kiasi hicho bado hakitoshi kwa klabu kubwa kama United.
Kwa sasa United wamebakiwa na alama 43 baada ya suluhu dhidi ya Burnley na kama Manchester City watafanikiwa kuibuka kidedea katika mchezo wao dhidi ya Newcastle baasi watakuwa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 15.

0 comments:

Post a Comment