Tuesday 5 December 2017

Muigizaji maarufu nchini India aaga dunia




Mwigizaji Kapoor, alitamba na filamu maarufu kutoka Bollywood kama vile Trishul (1978), Namak Halaal(1982), Deewar (1995), Kabhie Kabhie (1976) na nyingine nyingi, amekuwa akiugua kwa muda kabla ya kukutwa na mauti siku ya jana. Shashi anatoka katika familia ya vipaji ya Kapoor ambayo imetawala tasnia ya filamu za Kihindi kwa miongo mingi.
Katika enzi za uhai wake Kapoor alishawahi kushinda tuzo nyingi za filamu za taifa na alitunukiwa tuzo kuu ya heshima ya  Padman Bhushan inayotolewa na raia wa India mwaka 2011.
Mbali na filamu za kihindi Kapoor ameigiza pia na wasanii wengine kutoka Marekani, Uingereza na Urusi kama filamu ya Vozvrashcheniye Bagdadskogo Vora ya mwaka 1988.
Kwa mujibu wa mtandao wa Hindu Times, Kapoor amefariki kwa ugonjwa wa figo ambao ulikuwa unamsumbua kwa miaka mingi.
Tayari Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametoa pole kwa familia ya marehemu Kapoor kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter.
Jikumbushe hapa baadhi ya filamu zake alizowahi kuigiza enzi za uhai wake

0 comments:

Post a Comment