Friday, 15 December 2017

Nchi za Afrika zahamasisha ushirikiano na China katika kuimarisha Viwanda


Nchi za Afrika kusini mwa Sahara zinataka kuvutia uwekezaji na uhamishaji wa teknolojia kutoka China, ili kustawisha sekta ya viwanda ambayo imekwamishwa na ukosefu wa fedha na changamoto za raslimali watu.
Maofisa walioshiriki kwenye mazungumzo kuhusu kuhimiza uwekezaji kando ya Maonesho ya Ushirikiano wa Uwezo wa Viwanda kati ya China na Afrika yaliyofanyika huko Nairobi, wamesema mitaji ya China, ujuzi na uzoefu vinatakiwa kutumiwa kuendeleza viwanda barani Afrika.
Kiongozi wa Timu ya Kuhimiza Uwekezaji wa Kamati ya Uwekezaji ya Ethiopia EIC Bw. Aschalew Tadesse amesema, China imechukua nafasi ya kimkakati wakati nchi za Afrika zikianzisha ufufuaji wa viwanda.
Pia amesema, wawekezaji wa China wanakaribishwa kushiriki kwenye uzinduzi wa maeneo ya viwanda ambayo yanatarajiwa kuleta nafasi nyingi zaidi za ajira na kutengeneza bidhaa za kuuza nchi za nje.

0 comments:

Post a Comment