Thursday 14 December 2017

Rais wa Ufaransa ataka uharakishwaji wa maswala ya hali ya hewa

 

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameonya kuwa, jumuiya ya kimataifa inashindwa kwenye mapambano dhidi ya suala la mabadiliko ya hali ya hewa, na kutoa wito wa kuharakisha kuchukua hatua halisi kutekeleza makubaliano ya Paris kuhusu suala hilo.

Bw. Macron amesema hayo kwenye mkutano wa kutafuta uwekezaji wa operesheni ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa wenye kaulimbiu ya "Sayari Moja" ulioandaliwa na Ufaransa, Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia mjini Paris. Viongozi zaidi ya 60 wa nchi mbalimbali na wajumbe elfu 4 kutoka mashirika ya kimataifa, makampuni na taasisi mbalimbali wameshiriki kwenye mkutano huo.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres amesema, makubaliano ya Paris ni msingi wa mpango wa kimataifa kuchukua hatua yenye ufanisi zaidi kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea na mfuko wa fedha wa binafsi unapaswa kuwa sekta muhimu ya kutimiza lengo la kuzuia joto linaloendelea kuongezeka.

0 comments:

Post a Comment