Thursday 14 December 2017

UNICEF yasema watoto laki 4 wenye utapiamlo wanaweza kufariki nchini DRC



Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeonya kuwa watoto zaidi ya laki 4 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wako katika hali ya utapiamlo na kukabiliwa na hatari ya kufariki.
UNICEF imetoa taarifa ikisema, hali hiyo mbaya katika eneo la Kasai nchini humo inatokana na mabavu, kuharibiwa kwa makazi na kupungua kwa uzalishaji wa kilimo katika miezi 18 iliyopita.
Taarifa imesema, ingawa hali ya usalama imetulia katika baadhi ya sehemu za eneo hilo na baadhi ya watu waliokimbia makazi yao wameanza kurudi nyumbani na jamii zao, lakini hali ya kibinadamu bado ni mbaya.

0 comments:

Post a Comment