Thursday 14 December 2017

Real Madrid yafuzu fainali ya mashindano ya klabu bingwa duniani


Timu ya Real Madrid yafuzu fainali ya mashindano ya klabu bingwa duniani
Kufuatia ushindi wa magoli 2-1 iliopata jana ilipocheza dhidi klabu ya Al Jazira ya nchini umoja wa falme za kiarabu, Real Madrid imefanikiwa kufuzu mechi ya fainali ya klabu bingwa duniani itakayopigwa Disemba 16 mjini Abu Dhabi ambapo itapambana na mabingwa wa Amerika ya Kusini Gremio walioingia fainali baada ya kuwafunga Pachuka kutoka Mexico.
Magoli ya Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo likiwa ni la kusawazisha baada ya Al Jazira kutangulia na Gareth Bale aliyefunga la ushindi.
Kwa goli lake hilo, Ronaldo anaweka rekodi mpya ya ufungaji katika mechi za mashindano hayo akifikisha sita sasa amabyo ni zaidi ya Messi, Suarez na Delgado ambao kila mmoja ana magoli matano.

0 comments:

Post a Comment