Mkurugenzi
wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri picha
zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM
yana nyufa ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa
majengo makubwa.
Mwakalinga
amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za 'expansion joint'
ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo, lakini majengo hayo yamekidhi
vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake.
"Kila
design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint,
majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck
kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku
kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle,
hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu", amesema Bwana
Mwakalinga.
0 comments:
Post a Comment