Mbunge
wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amefunguka na kumjibu Spika
wa Bunge, Job Ndugai kuhusu kauli yake ya kusema kuwa utaratibu
uliotumika kumsafirisha Tundu Lissu kwenda Nairobi kuwa ulikwenda
kinyume na mfumo wa serikali na kibunge.
Tundu
Lissu anadai kuwa kauli hiyo haina ukweli hata kidogo kwani kitendo cha
yeye kusafirishwa kwa ndege mnamo Septemba 7, 2017 majira ya usiku
kuelekea kwa matibabu nchini Kenya ni wazi kuwa kibali kilitolewa na
serikali pamoja na Bunge kwani bila hivyo yeye asingeweza kusafirishwa.
"Mimi
sikuamua kuja Nairobi sikuwa najitambua, watu walioamua mimi kuja
Nairobi ni pamoja na Spika Ndugai mwenyewe watu wameniambia kwenye hicho
kikao cha nipelekwe wapi Ndugai alikuwepo, Naibu wake alikuwepo, Katibu
wa Bunge wakati huo Kashilila alikuwepo, Mwenyekiti wa chama changu
alikuwepo ile ndege iliondoka saa sita usiku sasa ingerukaje kama
haikuruhusiwa na serikali ya Tanzania kuruka kuja Nairobi? Kwa hiyo hii
habari ya kwamba amepelekwa wapi ni mambo ya kujishikiza shikiza tu ni
Bunge kujaribu kukwepa wajibu wake wa kisheria" alisema Tundu Lissu
Aidhaa
Tundu Lissu aliendelea kufafanua kuwa "Nimesema mimi siombi fadhila,
hakuna mtu anaomba kufadhiliwa hapa mimi naomba haki ambayo anatendewa
mtu aliye Mbunge anayeumwa ambaye amelazwa nje ya kituo chake cha kazi
hicho tu.
Mbali
na hilo Tundu Lissu amesikitishwa na upelelezi unaofanywa na jeshi la
polisi kuhusu shambulio lake la kutaka kuuawa na kusema anashangaa mpaka
leo jeshi la polisi halijasema linamshuku nani kuhusika na shambulio
hilo na mpaka leo jeshi la polisi halijaweza kumhoji japo aweze kutoa
maelezo yake.
0 comments:
Post a Comment