Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Dk John Magufuli ameendelea kusimamia
azma yake ya kumaliza rushwa ndani ya chama hicho.
Dk
Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano amesema CCM haitasita
kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu iwapo
itabainika rushwa imetumika.
Akifungua
mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo Jumatatu Desemba 18,2017 Rais
Magufuli amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa.
Amewataka wajumbe wa mkutano kuchagua watu waaminifu na wenye mapenzi ya dhati na CCM.
“Msichague
watu kwa urafiki au kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru
mzee Kikwete (Jakaya) yeye hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo
huenda mimi nisingepita,” amesema.
Rais
Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuvunja makundi yaliyojitokeza
wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho ulioanza Aprili, 2017.
“Vunjeni
makundi chaguzi zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM
haitamvumilia mtu mwenye kuendeleza makundi,” amesema.
0 comments:
Post a Comment