Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema
kuwa endapo Tume ya Uchaguzi na Serikali haitasogeza mbele uchaguzi
mdogo wa Wabunge unaotarajiwa kufanyika Januari 13, 2018 basi UKAWA
hawatashiriki uchaguzi huo.
Mbowe
amesema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya
UKAWA kuwa serikali pamoja na Tume ya Uchaguzi inapaswa kuahirisha
uchaguzi huo kwanza ili ifanyike tathmini na wadau wa siasa waweze
kuzungumza mambo mbalimbali ambayo wamejifunza kupitia uchaguzi mdogo wa
udiwani uliofanyika hivi karibuni kwani kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa
sheria, taratibu na haki za binadamu.
"Miaka miwili ya Rais Magufuli imetupa funzo kubwa sana kwamba mambo siyo sawasawa na sisi kukimbilia kwenda moja kwa moja kwenye uchaguzi katika mazingira haya tunaona kwamba tunaliingiza Taifa katika mpasuko mkubwa sana.

"Sisi
kama vyama vya upinzani tunaamini kabisa kuendelea na uchaguzi huu
tutakuwa hatulitendei haki taifa, sisi tunaamini katika hatua ya sasa
uchaguzi huu unastahili kuaihirishwa, hivyo ni rai yetu kwa serikali na
msimamizi wa uchaguzi kuona umuhimu wa kuarisha kwanza uchaguzi huu"
alisema Mbowe
Aidha
Mbowe aliendelea kusema kuwa endapo Serikali na Tume ya Uchaguzi
haitaiona umuhimu wa kuahirisha uchaguzi huo basi wao kama UKAWA
hawatashiriki katika uchaguzi huo wa Januari 13, 2017.
"Kuendelea kushiriki chaguzi za kuumiza watu, kufunga watu, chaguzi za kuvunja amani hazitujengi kama taifa bali tunaongeza mpasuko na ufa kati yetu, hivyo sisi rai yetu uchaguzi huu usogezwe mbele wadau tukae kwanza, vyama vya siasa tuzungumze hivi kweli tumechagua uchaguzi ukawe wa mapanga, visu na marungu, hivi kweli tumeshakubaliana mawakala watolewe vituoni?

"Tukishakubaliana
kuhusu haya na kwanini yalikiukwa ndiyo uchaguzi ufanyike. Kama Tume ya
Uchaguzi na Serikali itapuuza sisi UKAWA hatutakuwa tayari kushiriki
uchaguzi wa Januari 13, 2018" alisema Mbowe.
0 comments:
Post a Comment