MAMLAKA
ya udhibiti wa huduma za nishati na maji( ZURA ) imetoa taarifa juu ya
bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia leo Jumanne
tarehe 12-12-2017.
Akizungumza
na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara Kaimu Mkurugenzi
masuala ya wateja Mussa Ramadhani Haji alisema kuwa bei hizo Zura
imepanga kufuatia mambo yafuatayo;-
Wastani
wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations)
katika mwezi wa Novemba 2017 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia
mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa Disemba 2017.
Pia
thamani ya shillingi ya Tanzania , gharama za usafiri , Bima na’
Premium ‘hadi Zanzibar . Kodi za serikali na kiwango cha faida kwa
wauzaji wa jumla na rejareja.
Alisema
bei za rejereja ya mafuta ya Petroli kwa mwezi wa Disemba, 2017
imepanda kwa shillingi (100) kwa lita kutoka shilling 2,130 Mwezi wa
Novemba , 2017 hadi shilling 2,230 kwa lita katika mwezi wa Disemba ,
2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.5%.
Pia
alisema bei ya rejereja ya mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Disemba , 2017
imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shilling 2,280 kwa lita
katika mwezi Novemba hadi shilling 2,190 kwa lita katika mwezi wa
Disemba, 2017 sawa na asilimia 4%.
Aidha
alisema bei ya reja reja ya mafuta ya Taa kwa mwezi wa Disemb 2017
imepanda kwa shilling (80) kwa lita kutoka shillingi 1.539 kwa lita
katika mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 1,619 katika mwezi wa
Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.9%
Vilevile
bei ya reja reja ya mafuta ya Banka kwa mwezi waDisemba, 2017 imeshuka
kwa shilling (90) kwa lita kutoka shillingi 2,122 kwa lita katika mwezi
wa Novemba, 2017 hadi shilling 2,032 katika mwezi wa Disemba , 2017
sawa na ongezeko la asilimia 4.4%.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
0 comments:
Post a Comment